Kiingereza | Kifaransa | Kiswahili
Afrigen ni sehemu ya juhudi kubwa ya ujanibishaji, yaani kazi ya kutayarisha zana za kiteknolojia katika lugha za kiafrika, inayoitwa ANLoc (African Network for Localization / Mtandao wa Ujanibishaji kwa Afrika). Kwa kifupi, lengo la Afrigen ni kuandaa mandhari kwa lugha 100 za bara Afrika katika miezi 12. Mpaka leo hii, lugha 36 za Afrika, kutoka lugha 2000 kwa jumla, zinazo mandhari zao tayari.

Mandhari kwa sababu gani?

Ngazi ya kwanza katika ujanibishaji wa lugha yoyote ni kuhakikisha kwamba watumiaji wote na mifumo ya tarakilishi zote inaweza kutambulisha vipengele kwa kufuatana na lugha na nchi. Mandhari ni faili kuu ambalo linaweza kutumiwa katika matumizi mbalimbali kama vile kutamka data ya msingi kwa kila jozi ya lugha/ nchi. Data inajumlisha taarifa kuhusu lugha, k.m. namna ya kuelezea tarehe na maandishi, vile vile za nchi kama majina na alama za hela. Mandhari yakiandaliwa sawa, lugha ya kila nyaraka itaweza kutambulishwa, itakayorahisisha mambo kama vile utafutaji, uchagizi tahajia, na vipimo maalum vya watumiaji katika programu kadhaa. Kumaliza mandhari kwa lugha fulani ni msingi wa maendeleo na shughuli zote za ujanibishaji kwa lugha hiyo.

Nisaidiaje?

Ukisema lugha yoyote ambayo haijamalizwa katika orodha hii (yaani, kuna mapande mekundu pembeni ya jina la lugha), na ukiweza kujitolea masaa mawili au matatu ili kuhakikisha kwamba lugha yako iingie ulimwengu wa kiteknolojia, tafadhali wasiliana nasi katika locales@africanlocalization.net.
100 African Language Locales
View SlideShare presentation or Upload your own. (tags: africa language)